Habari za Mastaa

Ifahamu stori iliyomkutanisha D’Banj na Kanye West mpaka kutengenezwa kwa ‘Oliver Twist’!

on

Kati ya ngoma kubwa za staa wa muziki kutoka Nigeria, D’Banj huwezi kuacha kuitaja hit song ya Oliver Twist… Nimekutana na interview ya D’Banj na jarida la Forbes Africa (December 2015) na kikubwa kilichonigusa ni stori iliyompelekea mpaka kukutana na Kanye West na hatimaye kupata mchongo wa kutengeneza ‘Oliver Twist’ single yake ya kwanza chini ya G.O.O.D Music lebo inayomilikiwa na Kanye West.

BANJ3

D’Banj.

>>> “Kanye West na mimi tulikutana kwa bahati mbaya… nilikuwa Dubai  na crew yangu tukisubiri kubadilisha ndege, tukiwa tunasubiri wahudumu kadhaa wa ndege wakaja kwangu kwa spidi huku wakiita ‘Mr Kanye West’… nikashangaa na kujitazama juu mpaka chini na kisha nikawatazama na waliponikaribia nikatoa mkono na kuwaambia ‘mambo naitwa D’Banj lakini kama nafanana na Kanye West basi inamaanisha yupo maeneo haya..’. Tukaanza kumtafuta na tulipompata tukamuelezea kilichotokea na hapo ndipo kila kitu kilipoanzia… Nilikutanishwa na Kanye baada ya wahudumu wa ndege kunifananisha naye...” <<< D’Banj.

BANJ4

Kanye West.

Baada ya D’Banj na Kanye West kukutana Airport, Dubai, wawili hao waliongea mengi na D’Banj akatumia fursa hiyo kumsikilizisha Kanye baadhi ya kazi zake… baada ya rapper huyo wa Marekani kuvutiwa na midundo ya D’Banj mastaa hao wakapeana namba kisha wakaachana…

>>> “Baada ya kukaa na kuzungumza naye mambo mengi, akaomba tubadilishane namba… nikampatia yangu akanipatia yake tukaachana. Baada ya wiki kadhaa akanipigia na kuniomba niende Los Angeles kwa mazungumzo zaidi, nilipofika huko Kanye akanitambulisha kwa mastaa wenye majina makubwa kwenye muziki kama Big Sean, Pusha T, Hit-Boy na LA Ried… tukasign mikataba na siku chache badaaye tukarekodi ‘Oliver Twist’…” <<< D’Banj.

SONY DSC

Single ya Oliver Twist ilimpa D’Banj mafanikio makubwa kwenye levo za kimataifa pamoja na kukuza jina lake kwenye nchi kama Uingereza na Marekani… na kwa sasa single ya ‘Oliver Twist’ inagusa watazamaji milion 36, 422, 917 kwenye mtandao wa YouTUBE ikiwa ni moja ya videos za wasanii wa Africa ziliyotazamwa zaidi!

OLIVA

Itazame Oliver Twist kwenye hizi dakika tatu hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.Soma na hizi

Tupia Comments