Mkuu wa Wilaya ya Chato, Bi.Matha Mkupasi amemuagiza Mwenyekiti wa Kijiji kitela kata ya chato kuhakikisha anaitisha vikao mara moja pamoja na wananchi ili kukomesha vitendo vya kishirikina vinavyoendelea ndani ya wilaya ya Chato mkoani Geita.
Akitoa Maagizo hayo wakati wa ufunguzi na Makabidhiano ya nyumba za watumishi wa Afya kutoka hospitali ya kanda ya chato zipato nyumba 27 zilizojengwa kuanzia mwaka juzi zenye thamani ya shilingi Milioni 860 .
” Huku ni kwa wananzengo asilimia 100 mwenyekiti uko hapa hawa ni watumishi ambao tunawahitaji sisi waje watupe huduma watoe huduma kwa wananchi wetu tusipo weka ushirikiano utashangaa baada ya mwaka mmoja na miezi kila mtu anataka kuhama ñinasema hivi kwa sababu baadhi ya maeneo ukienda mwalimu anakwenda kukaa siku mbili anasema mara usiku nimekabwa mara sijui niliacha laptop imezima nimekuta inawaka yakianza hayo watumishi watakimbia niombe tufanye mikutano kule, “Mkuu wa Wilaya