Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo amefanya ziara katika Shule ya Msingi Toangoma huu ukiwa ni mwendelezo wa kuifahamu Wilaya ya Temeke na maeneo yenye changamoto zaidi ili kuweza kuona ni jinsi gani zinaweza kutatuliwa.
Jokate amefanya ukaguzi wa madarasa yanayoendelea kujengwa Shuleni hapo na kusikiliza changamoto zinazoikabili Shule hiyo yenye Wanafunzi zaidi ya Elfu nne.
DC Jokate ameagiza Manispaa impelekee mpango wa kupunguza changamoto ya miundombinu kwa angalau asimilia 50 wilaya nzima tofauti na mpango waliokuwa nao sasa ambao bado hajaridhishwa nao.
“Ni lazima kuwe na mkakati madhubuti na endelevu kwasababu kila mwaka idadi ya Wanafunzi inaongezeka, naiomba Manispaa ishirikiane na Viongozi wa maeneo husika pamoja na Wanachi ili mpango uwe shirikishi”——Jokate Mwegelo