Mkuu wa Wilaya Kilombero Mkoani Morogoro Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwenye vyombo vya sheria ikiwemo mahakama ili haki iweze kutendeka kwa watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto.
Dc Kyobya amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria ambayo yamemeanza kuadhimishwa january 25 mwaka huu hadi 1/ 2/ 2025 .
Dc kyobya amesema changamoto kubwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakifumbia macho vitendo hivyo ambayo vinaharibu vizazi, wengine wakipata ujauzito katika umri mdogo na kukatishwa ndoto zao za kielemu.
Amesema wiki ya sheria itumike kutatua changamoto mbalimbali za kisheria ambazo zinawakabili wananchi ikiwemo Migogoro ya ardhi ,mirathi, ukatili, na Migogoro ya kifamilia.
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kilombero Mhe. Regina Futakamba amewataka wananchi kujitokeza Kwa wingi Ili kupata elimu ya masuala ya kisheria.
Amesema elimu hii itasaidia kwenye masuala ya ufunguaji wa mashauri mahakamani pamoja na njia mbalimbali za kuzipata haki kwenye vyombo vya sheria.
Nao wakazi wa Ifakara wamesema ufikiwaji wa elimu hiyo utasaidia wananchi kutambua mambo ya sheria hasa Vijijini kwenye wananchi wengi ambao hawana uelewa wa masuala hayo.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya Mji wa ifakara.