Top Stories

DC Mbeya apiga marufuku PA za misiba Mbeya

on

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt. Rashid Chuachua amepiga marufuku magari yanayofanya matangazo ya misiba jijini hapa baada ya kuchukua miili ya watu waliofariki dunia hospitalini, akisema yamekuwa yakileta hataruki kwa wananchi na kujenga hofu.

Chuachua amesema hayo leo Jumanne Agosti 10, 2021 huku akiiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya doria na kuwachukulia hatua wamiliki wa magari hayo watakaobainika.

“Kumekuwa na tabia ya familia za watu wanaopoteza maisha kukodi magari ya matangazo na kuanza kutangaza maeneo mbalimbali ya jiji na kutaja majina ya wapendwa wao, sasa kwa niaba ya mkuu wa mkoa nimepiga marufuku rasmi leo Agosti 10 2021,” Dk Chuachua.

MESSI MALAIKA MOTONI, GENGE LA UHALIFU, MAAJABU YA BIBI YAKE, LAANA YA BABU YAKE

Soma na hizi

Tupia Comments