Top Stories

DC Mtwara kuzikwa na Watu kumi “Serikali itasimamia, hatusafirishi mwili, lini na wapi sio muhimu” (+video)

on

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Mtwara, Evod Mmanda yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10 na Serikali ndio itasimamia mazishi hayo na kwamba mwili hautosafirishwa.

“Familia ya Marehemu imeridhia mwili kutosafirishwa hivyo mazishi yatafanyika hapa Mtwara, lini na wapi sio muhimu sana kwasababu itawahusu Watu hao kumi watakaoshiriki” – RC Mtwara

KIFO CHA DC MTWARA, WAZIRI JAFO AELEZA KILICHOMUUA “ALIKUWA NA CHANGAMOTO YA UPUMUAJI”

Tupia Comments