Top Stories

DC Sabaya aibukia mochwari apiga marufuku maiti kuzuiwa kisa madeni (+video)

on

Serkali Wilayani Hai imepiga marufuku masharti yanayowekwa na Hospitali ya kuzuia miili ya watu waliofariki hadi Ndugu zao watakapomaliza madeni yanayotokana na matibabu wakati wa uhai wake.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameelekeza kutowekwa sharti lolote wakati wa kuchukua mwili na kuongeza kwamba utaratibu huo unaongeza huzuni na majonzi kwa wafiwa.

Amesema inashangaza kuona huu utaratibu unakita mizizi huku ukiwa hauendani na Mila na Desturi za kibinadamu.

Sabaya pia ameonya Watumishi wa Afya kuacha kuwekeza katika kufitiniana na majungu kwani kunaua na kuondoa Watu wenye uwezo katika Taasisi na kubakiza Watu ambao wamewekeza katika maneno tu.

Soma na hizi

Tupia Comments