Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma Sophia Kizigo amewataka vijana wanaotumia dawa za kulevya hasa bangi kuacha matumizi hayo kwani ni ushamba na inahatarisha Afya ya kijana ambaye ndio nguvu kazi ya Taifa.
Kizigo amesema hayo katika Tamasha la Kijana lililofanyika katika kijiji cha Kibakwe wilaya ya Mpwawa mkoani Dodoma na mgeni rasmi akiwa George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe.
“Kuna rafiki zetu wengi ni wavuta bangi hapa huo sio ujanja kijana wa mama Samia na kijana anayejielewa,kijana anyejitambua havuti bangi anajishughulisha na kama uko shuleni unasoma ndugu zangu vijana wenzangu tuepuke madawa ya kulevya kwa Afya na nguvu kazi ya Taifa na viajan wenzangu haswa wa Mpwapwa tuacha matumiazi ya bangi kuvuta bangi ni ushamba” Sofia Kizigo mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
Akizungumza na wananchi wa Mpwapwa George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amewaomba wananchi kuachana na kilimo na biashara ya Bangi hasa katika wilaya ya Mpwapwa