Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, Ngollo Malenya ameungana na Wananchi site kwa kazi za kujitolea pamoja na Wanakijiji hao kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mputa ambayo tangu kupatikana kwa Uhuru haikuwahi kuwa na Shule ya Sekondari.
Wilaya ya Namtumbo imepata fedha Tsh. 560,552,827 ajili ya ujenzi wa Shule hiyo
DC amesema “Hii miradi tunayopewa ni sehemu ya kutatua changamoto za Wananchi wetu, kwahiyo naomba Wananchi wachukulie ni miradi yao, washiriki kikamilifu na kuhakikisha inaisha kwa wakati ili Watoto wetu wasikutane na adha yoyote”