AyoTV

VIDEO: Mtazame Mkuu wa Dar es salaam akitoa maagizo matatu makubwa April 12

on

April 12 2016, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa maagizo kwenye mambo matatu wakiwemo ombaomba wa mabarabarani, majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipo kuwa na parking na wamiliki wa bar kupiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.

Paul Makonda ametoa siku sita mpaka April 18 2016 Ombaomba wote ndani ya Dar es salaam kuondoka barabarani, wamiliki wa majengo walipe faini na kuweka utaratibu wa magari kupata parking au kubomoa majengo yao na kuhusu wamiliki wa Bar Paul Makonda amezungumza pia.

Amesema >>> ‘wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika, mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe’ – Paul Makonda 

 Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments