Michezo

De Gea amfukuza Casillas Real Madrid.

on

LANDOVER, MD - JUNE 07:  Iker Casillas of Spain comes off by David de Gea of Spain during an international friendly match between El Salvador and Spain at FedExField on June 7, 2014 in Landover, Maryland.  (Photo by David Ramos/Getty Images)

LANDOVER, MD – JUNE 07: Iker Casillas of Spain comes off by David de Gea of Spain during an international friendly match between El Salvador and Spain at FedExField on June 7, 2014 in Landover, Maryland. (Photo by David Ramos/Getty Images)

 

Huku taarifa zikizidi kumiminika kuhusu kllabu ya Real Madrid kukaribia kumsajili kipa David De Gea wa Manchester United , taarifa nyingine zimeibuka zikimhusisha kipa namba moja wa klabu hiyo Iker Cassilas na kuihama klabu hii ambayo ameitumikia kwa muda mrefu .

Cassilas inasemekana kuwa amefikia uamuzi wa kuondoka klabuni hapo ili kuepusha tatizo ndani ya klabu hiyo linaloweza kusababishwa na vita ya kuwania namba kati yake na David De Gea wakati kipa huyu wa zamani wa Atletico Madrid atakaposajiliwa .

Real Madrid tayari imefikia uamuzi wa kumsajili De Gea na ishara zote zinaonyesha kuwa kipa huyu anaelekea kuwa kipa namba moja ndani ya Santiago Bernabeu na Cassillas ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akicheza chini ya kiwango chake cha kawaida amejiandaa kuondoka .

Ripoti iliyonukuliwa toka kwenye Televisheni ya Taifa ya Hispania inasema kuwa Real Madrid imemuandalia Cassilas mchakato wa kuihama klabu hiyo kwa heshima kwani inathamini mchango wake .

Cassillas alianza kuitumikia klabu hii tangu akiwa na umri mdogo ambapo alipata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umi wa miaka 19 akicheza kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ambapo aliingia kuchukua nafasi ya kipa aliyeumia .

Cassillas amekuwa kipa namba moja kwa muda wote tangu alipoanza kuingia kwenye kikosi cha kwanza akitokea kwneye kikosi cha vijana na ni misimu miwili iliyopita pekee wakati alipopoteza nafasi yake kwa kipa Diego Lopez kufuatia jeraha alilopata .

Tupia Comments