Juventus wako tayari kumsajili beki wa Chelsea Renato Veiga kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.
Klabu hiyo ya Italia imekubali kugharamia mishahara ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno na kulipa ada ya mkopo ya £3.8m.
Hakuna chaguo la kununua limejumuishwa katika mpango huo.
Veiga alijiunga na Chelsea pekee kwa mkataba wa £11.8m mwezi Julai akitokea klabu ya Uswizi Basel.
Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vilisema alikua akichanganyikiwa kucheza katika nafasi ya beki wa kushoto, akipendelea kutumika katika nafasi ya beki wa kati.
Chelsea wanaamini atapata dakika zaidi nchini Italia huku mchezaji huyo akiwa na hamu ya kusalia kwenye kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Kombe la Dunia la 2026.
Juventus wamewashinda wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Borussia Dortmund katika usajili wa Veiga.
Meneja wa Chelsea Enzo Maresca alikuwa amemtaka Veiga kusalia wiki iliyopita, akisema: “Ikiwa kuna mchezaji ambaye anataka tu kucheza katika nafasi moja, watapata tabu.”
Veiga ameanza mara moja tu Ligi ya Premia msimu huu katika mechi 18 katika mashindano yote.