Michezo

Arsenal waiua Napoli Europa League robo fainali

on

Leo Alhamisi ya April 11 2019 baada ya kumalizika kwa michezo ya round ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League, leo ilikuwa ni zamu ya kuangalia michezo minne ya robo fainali ya UEFA Europa League iliyochezwa katika viwanja mbalimbali Ulaya.

Arsenal ambao bado wamekuwa hawatabiri kutokana na kukosa muendelezo mzuri wa kupata matokeo chanya kila kukicha, wamewashangaza watu baada ya kuipiga Napoli 2-0, zilizofungwa na Ramsey dakika ya 14 na Koulibaly wa Napoli akajifunga dakika ya 25.

Hivyo Arsenal sasa katika mchezo wa marudiano nchini Italia watalazimika kuhakikisha kuwa wanapata walau sare ya yoyote ile itawavusha kucheza nusu fainali au kupoteza kwa chhini ya goli, hii imeanza kuleta matumaini kuwa Arsenal wanaweza kuishangaza Napoli.

Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys

Soma na hizi

Tupia Comments