Top Stories

Defao azikwa DR Congo

on

Mwili wa Mwanamuziki François Lulendo Matumona maarufu General Defao hatimaye umezikwa siku ya jana Jumamosi nchini DR Congo.

Defao alifariki mwezi Desemba mwaka jana katika hospitali Laquintinie huko Douala, Cameroon, ambako alikuwa akipokea matibabu.

Watu wa karibu wanasema mwanamuziki huyu hakuacha mtoto lakini ameacha vitu vya vya thamani (mikufu ya dhahabu aliyokuwakuwa akivalia shingo).

Wanamuziki na mashabiki wake waliohudhuri mazishi hayo, wakiwa wamevalia mavazi ya bei ghali wanadai Defao alikuwa mmoja wao wa kuvaa mavazi ya ghali.

Soma na hizi

Tupia Comments