Michezo

David De Gea mikononi mwa Real Madrid?

on

D42F627BF19646BD840257CACAAC7B97.ashx

Klabu ya Real Madrid imeweka mpango wa kumsajili kipa wa kimataifa wa Hispania David De Gea ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Manchester United ya England.

De Gea kwa muda mrefu ametajwa katika mipango ya usajili ya Real Madrid lakini kwa sasa Madrid wanaonekana kuthibitisha kile ambacho kimezungumzwa na vyombo vya habari barani ulaya .

Magazeti Uingereza hayajapitwa na hii story, yameandika kwamba Bodi ya Real Madrid imekaa na kujadili usajili wa kipa huyu ambapo imesemekana kuwa klabu hii inajiandaa kupeleka ofa ya kwanza kwa United na imejiandaa kupokea majibu ya hapana!

Real Madrid inajiandaa kumbadili kipa wake wa muda mrefu Iker Cassillas ambaye kwa sasa anaonekana kushuka kiwango.

Real Madrid inajiandaa kumbadili kipa wake wa muda mrefu Iker Cassillas ambaye kwa sasa anaonekana kushuka kiwango.

Madrid imesema kuwa haitakuwa tayari kulipa fedha nyingi kuliko kawaida endapo United itataka fedha nyingi na badala yake wanajindaa kumsubiri De Gea hadi hapo mkataba wake utakapomalizika ili kumsajili bila gharama yoyote.

Endapo haitampata De Gea Real Madrid imejipanga kuzungumza na Chelsea juu ya usajili wa kipa raia wa jamhuri ya Czech, Petr Cech ambaye klabu hiyo ya London imemuweka sokoni kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.

Real Madrid inamtazama  De Gea kama mrithi wa muda mrefu wa kipa namba moja wa Hispania, Iker Cassillas ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akicheza chini ya kiwango mpaka kulaumiwa na watu wengi.

Kaa karibu na millardayo.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa>twitter Insta Facebook

Tupia Comments