Mshambuliaji wa kimataifa wa Serbia anayeichezea Simba SC Dejan Georgijevic (28) leo ametangaza kuwa amevunja mkataba wake wa Simba SC, Dejan ameeleza hayo ikiwa ni siku 53 zimepita toka ajiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu na kumfanya kuwa mchezaji mwenye mkataba mrefu zaidi Simba SC.
Dejan ameeleza kupitia instagram account yake ameeleza kuwa Simba SC wamekuwa wakikiuka vitu vingi walivyokubaliana kwenye mkataba wao hivyo ni Simba SC ndio wamevunja mkataba.
“Nathibitisha kuwa mkataba wangu wa ajira Simba SC umevunjwa kwa sababu vimekiukwa na club vitu vingi vya msingi kimkataba, asante mashabiki kwa sapoti na mapenzi yenu mliyonipa”>>> Dejan Georgijevic
Kwa upande wa Simba SC hatujampata afisa habari wao Ahmed Ally aweze kutolea ufafanuzi zaidi