Mix

Mwanamke Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya New Delhi India

on

Mamlaka kwenye mji wa New Delhi India zimethibitisha kwamba zimewakamata Wanawake wawili wa Kiafrika baada ya kuwakuta na dawa za kulevya kilo nne.

Mamlaka zimesema katika Wanawake hao kuna Mtanzania mmoja aitwae Pamela D. Kirrita mwenye umri wa miaka 41 na mwingine ni Mzambia Thelma Mkandawire mwenye umri wa miaka 38.

Ripoti iliyotolewa na mamlaka hiyo imesema Wanawake hao walikamatwa kwenye hoteli moja karibu na uwanja wa ndege kwenye mji wa New Delhi na baada ya kupekua rekodi zao ikagundulika Pamela amewahi kuitembelea India mara 9 toka mwaka 2006 na amewahi kuzitembelea nchi nyingine kama Kenya na Ecuador.

Mtanzania Pamela Kirrita ametajwa alikua akifanya kazi chini ya raia mmoja wa Afrika Kusini wakati Mzambia Thelma hii sio mara yake ya kwanza kukamatwa, alishakamatwa mwaka 2015 huko Pakistan kwenye ishu hizohizo za dawa za kulevya.

Kitengo cha upelelezi kilianza kumfatilia Mzambia huyo baada ya kutua uwanja wa ndege New Delhi akitokea Sao Paulo Brazil kupitia Addis Ababa Ethiopia.

Ripoti hii imetolewa na Mamlaka za kupambana na dawa za kulevya India

ULIPITWA? Bonyeza hapa chini kumsikiliza Mfungwa aliyeibia simu Gerezani China na kumpigia simu Millard Ayo

ULIPITWA? Bonyeza play hapa chini kusikiliza kutoka Gerezani China barua ya Mtanzania Jackie Cliff aliyomuandikia Millard Ayo ili aisome kwa Watanzania

 

Soma na hizi

Tupia Comments