Top Stories

“Dereva aliegonga wanafunzi na kukimbia ajisalimishe” Muliro

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemtaka Dereva aliyewagonga Wanafunzi na kisha kukimbia, ajisalimishe haraka iwezekanavyo kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na yeye kwani hana uwezo wa kujificha zaidi ya saa 48.

“August 09, 2021 saa 11:15 Alfajiri katika Barabara ya Bagamoyo maeneo ya Afrikana Stendi ya Daladala Wilaya ya Kinondoni gari aina ya Scania liliwagonga watambea kwa miguu wawili (Wanafunzi) waliofahamika kwa majina ya Collins Ngowi (15) Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Makongo na Salvina Otieno (anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 10-15) Mwanafunzi wa darasa saba Shule ya Msingi Mount Sery (wote wawili baadae walifariki dunia)”

“Mwanafunzi mwingine aitwaye Ashura wa kidato cha tano Shule ya Sekondari Al-hara main alipata majeraha sehemu za mwili na alikimbizwa Hospitali, chanzo cha ajali kinachunguzwa ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa gari hilo, Dereva amekimbia baada ya kuwagonga Wanafunzi hao na tunamtafuta, ajisalimishe” ———-Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM

MESSI MALAIKA MOTONI, GENGE LA UHALIFU, MAAJABU YA BIBI YAKE, LAANA YA BABU YAKE

Soma na hizi

Tupia Comments