Top Stories

Dereva taxi arudisha Milioni 800 kwa abiria

on

Kuna hii ambayo imetokea Uturuki ambapo Dereva teksi huko Istanbul, amemrudishia abiria aliyesahau Euro 300,000 (zaidi ya Sh milioni 800 za Kitanzania) alizokuwa amezisahau katika gari lake.

Dereva teksi huyo, Olgaç alimpakia abiria huyo wa kigeni kutoka uwanja wa ndege wa Istanbul na kumpeleka hotelini.

Wakati akiondoka ndipo alipoona begi katika kiti cha nyuma na kugundua kuwa lilisahauliwa na abiria yule, Dereva Olgaç akaona kuwa kulikuwa na hela katika begi hilo.

Aliamua kupiga simu kwenye hoteli aliyomuacha abiria yule akawasiliana naye na kumpelekea begi lililokuwa na Euro 300,000.

Ni nadra sana kuona dereva mwaminifu kama huyo, hasa katika Jiji kubwa kama Istanbul, watu wengi wameshangazwa na kufurahishwa na jambo hilo.

GARI YA KANISA YAUA WATU SITA ARUSHA AKIWEMO PADRI “ILIGONGA GARI KWA NYUMA”-POLISI

 

Soma na hizi

Tupia Comments