Top Stories

Dereva Uber ashambuliwa na abiria

on

Mwanaume mmoja ambae ni Dereva wa Uber huko Darrien Connecticut Marekani aitwae Sijo George ametangaza kuacha kuifanya kazi hiyo baada ya kushambuliwa na Abiria aliyekua amembeba usiku, Sijo anasema camera zake za kwenye gari zilirekodi kila kitu kama inavyoonekana kwenye video hii.

Sijo anasema alipakia Abiria wawili Wanaume ambao walikua wanakwenda sehemu mbili tofauti lakini alipofika sehemu ya kwanza kushusha mambo yalibadilika kwa Abiria wote wawili kushuka na mmoja wao akasogea nje ya mlango wa Dereva na kumtaka amuoneshe leseni ambapo sekunde chache baadae Sijo aliambulia kipigo.

Sijo aliwapigia simu Polisi kupitia 911 na walifika eneo la tukio ambapo hata hivyo walitoa taarifa baadae kwamba wamemtambua Abiria aliefanya shambulizi hilo lakini hawajamkamata.

MORRISON HOI KWA KICHEKO BAADA YA YANGA KUFUNGWA “SISI TUNA WATU”

Soma na hizi

Tupia Comments