Mix

Wapendanao waliokubali kufa Jangwani ili kumwokoa mtoto wao.. (+Video)

on

dubai-desert-2

Mtu na mpenzi wake walianza safari ya Kutalii Jangwani wakiwa na mtoto wao pamoja na akiba kidogo ya maji ya kunywa wakiwa kwenye safari yao Jiji la New Mexico Marekani ambapo walikuwa wanatembelea eneo la Jangwa la White Sands National Monument.

Katikati ya safari mambo yakabadilika, maji yalibaki kidogo na wote walikuwa na kiu kutokana na Joto kupanda na kufikia Nyuzijoto 100, wakaamua kumpa mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka tisa maji yote ili abaki salama, baadae hali ikawaelemea na wote wawili wakafariki na kumuacha mtoto akiwa hai pekeyake.

Mtu na mpenzi wake waliofariki, Ornella Steiner ambaye ni mwanamke na mpenzi wake David Steiner wote ni raia wa Ufaransa walikutwa wakiwa wamefariki katika Jangwa hilo ambapo uchunguzi unaonesha wote wawili waliishiwa kabisa maji mwilini, lakini mtoto alifanikiwa kutoka salama na kuwahishwa Hospitali kutokana na hali yake kutokuwa nzuri pia kutokana na kuonekana kukutwa akiwa amedhoofu.

Wa kwanza kuanguka kutokana na kuishiwa maji alikuwa mwanamke, Ornella… lakini baba na mtoto wake wakajikongoja kwa umbali kidogo kama futi 2,000 mbele, baba naye akaishiwa nguvu na kuanguka akabaki mtoto pekeyake.

 Stori hiyo iko pia kwenye hii video hapa

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments