Habari za Mastaa

Kundi la Beyonce, Kelly na Michelle; ‘Destiny’s Child’ kurudi na Album mpya, Tour je?!

on

Imepita miaka 11 toka kundi la Destiny’s Child, linaloundwa na Beyonce Knowles, Kelly Rowland na Michelle Williams liachie album yao ya mwisho mwaka 2004 iliyopewa jina ‘Destiny Fulfilled’… leo ni mwaka 2015, je kundi hilo lina mpango wowote wa kuungana na kurudi studio?

DC 1

Mathew Knowles, baba yake Beyonce ambae pia alishawahi kuwa manager wa Beyonce mpaka mwaka 2011.

Mathew Knowles ambaye ni baba yake mzazi na Beyonce alishawahi kuwa manager wa kundi la Destniy’s Child aliuambia mtandao wa The Huffington Post, kuwa bado anajihusisha na projects nyingi za wasichana hao watatu na kwa sasa “yupo anaifanyia kazi” mipango na projects kadhaa za kundi hilo.

>>> “Nina matumaini makubwa sana kuwa hawa wadada wataungana tena na kurudi na album pamoja na world tour hivi karibuni… kwa sasa nipo nazifanyia kazi baadhi ya projects za Destiny’s Child, natengeneza pia autobiography ya Destiny’s Child… licha ya hayo, kwa sasa bado nipo kwenye mazungumzo na vituo mbalimbali  vya TV kuhusu uwezekano wa kutengeneza kitu kama tamthilia inayohusiana na kundi Destiny’s Child.”<<< Mathew Knowles.

DC 5

Mathew Knowles amesema kuwa alipokea pia barua pepe kutoka kwa mmoja ya wasichana wanaounda Destiny’s Child, Michelle Williams iliyosema kuwa yupo tayari siku yoyote kuungana na wenzake kwa ajili ya kurekodi album mpya… lakini issue inakuja kwa Beyonce mwenyewe… Je, atakubali kuungana tena na baba yake baada ya kumfukuza kazi kama manager wake mwaka 2011?!

Beyonce Knowles bado hajatoa neno lolote kuhusu hili.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments