Michezo

Usiku wa Europa League October 24

on

Baada ya kumalizika kwa michezo ya UEFA Champions League sasa ni muda wa kuenjoy na UEFA Europa League licha ya baadhi ya watu kuleta utani kuwa Ligi hiyo ni Ligi ya wanyonge kutokana na hupatikanaji wa timu shiriki.

Pamoja na hayo usiku wa leo zinachezwa timu pendwa katika Europa League ikiwemo Arsenal na Man United ambazo hazikupata nafasi ya kucheza Champions League kwa msimu wa 2019/2020.

Marcus Rashford ambaye amekuwa na mfululizo wa kupachika Magoli muhimu kwa timu ya Taifa ya England na Man United kwa hivi karibuni, msimu huu wa 2019/2020 imemtambulisha upya kinda Marcus Rashford Kama mmoja ya Nyota vijana wakutazamwa Sana katika Soka Ulimwenguni kwa Sasa.

Rashford siku ya Alhamisi atakuwa na mtihani wa kuitetea Man United dhidi ya Partizan Beograd katika mchezo wa Europa League unaochezwa saa 19:55 kuoneshwa kupitia ST World Football pamoja na game ya Arsenal itakayochezwa saa 22:00 EAT dhidi ya Victoria Gumares katika uwanja wa Emirates.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments