Ni kutoka Mahakamani Kisutu Dar es salaam ambapo post hii inamuhusu Mfanyabiashara James Rugemarila anaekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha.
Leo Rugemalila ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.
Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Rugemalila leo pia alidai kuwa anahitaji apate ushirikiano kutoka kwa upande wa Jamhuri ili wamjue na kumtaja ni nani mwizi wa Bil.309 za Serikali ambapo Wakili wa utetezi Balomi amedai kuwa hali ya Washtakiwa kiafya sio nzuri hasa Seth, hivyo upelelezi ukamilishwe kwa haraka ama wawe wanaelezwa hatua ilipofikia.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi December 22, 2017 ambapo ameutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi.
Ulipitwa na hii? Wamiliki IPTL/ESCROW wamefikishwa tena Kisutu leo, Maamuzi ya Mahakama je?