Mwanamke mmoja nchini Uingereza, ambaye ametambuliwa kwa jina la Sarah amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini humo baada ya kujifungua mtoto baaada ya kuugua saratani ya matiti.
Kutokana na ugonjwa huo madaktari walimwambia kuwa hawezi tena kushika ujauzito na kuzaa mtoto, na kwamba nafasi yake ya kuzaa ni asilimia 1 tu, lakini cha kushangaza ni kwamba alipata mimba tofauti na madaktari walivyotegemea.
“Niliambiwa kuwa kutokana na saratani hiyo ovari zangu zingezeeka ndani ya miaka mitano na katika umri wa miaka 32 hizo taarifa zilikuwa kubwa na za kuogopesha sana.” – Sarah
Baada ya matibabu yake ya saratani, Sarah alifanyiwa kipimo cha MRI kuangalia saratani hiyo kwa kiwango cha pili na ndipo madaktari walipogundua kuwa tayari ana ujauzito.
Kutokana na ‘muujiza’ huo mtoto huyo ambaye wazazi wake wamempa jina la Monty, pia watu wanamuita ‘mtoto wa muujiza’.
“Haya ndio mazingira yaliyotumika kufanya uhalifu” –Polisi Dodoma
BREAKING: ACT Wazalendo wazungumzia Wanachama wake 12 kuhamia CCM