Vigogo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga wanaendelea kusota rumande kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.
Wakili wa serikali, Leornad Chalo amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi bado haujakamilika hivyo akaiomba mahakama hiyo iahirishe kesi hadi tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, 2018 kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Dk. Tenga, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka kwa pamoja washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa la kutakatisha fedha Dola za Marekani 3,282,741.12, huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la udanganyifu.
Washtakiwa kesi ya kula njama, kulaghai na kujipatia fedha Bil.10. 73, Wamefikishwa Mahakamani.
Watuhumiwa wa ugaidi Arusha wavua nguo Mahakamani