Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na kinachodaiwa kuwa ukosefu wa amani katika chuo hicho kutokana na wanafunzi kukabiliana na polisi mara kwa mara wakiandamana na hivyo kuhatarisha usalama.
Taarifa ya seneti ya chuo hiyo imeeleza kuwa asubuhi ya leo walitoa tangazo kwa wanafunzi wa chuo hicho kuchukua mizigo yao na kuondoka kwenye maeneo ya chuo mpaka hapo uongozi wa chuo utakapo jiridhisha kukifungua chuo hicho tena.
Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino. Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.
Ulipitwa na hii? Sababu za gharama ujenzi reli ya kisasa awamu ya pili kuwa juu tofauti na ya kwanza
Hii je? JKCI yaadhimisha siku ya moyo duniani