Top Stories

Binti afukuzwa kazi kisa picha ya Instagram

on

Binti mmoja  nchini Marekani ambaye ni mchezaji mziki kwenye mechi mbalimbali za michezo (cheerleader) ameishtaki Ligi ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Marekani baada ya kumfukuza.

Binti huyo Bailey Davis amefungua mashtaka hayo baada ya timu hiyo kumfukuza kazi kutokana na picha ambayo alii-post kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram kwa madai kuwa ilikuwa kinyume na maadili yao.

Binti huyo ambaye amefanya kazi kama cheerleader kwenye ligi hiyo kwa miaka mitatu ameeleza kuwa ndoto zake zimezimwa ghafla kutokana na picha ambayo wanadai ni mbaya na hivyo hana budi kudai haki kwenye vyombo vya sheria.

Image result for cheerleader Bailey Davis. fired over instagram post

Steve Nyerere kafunguka “Wenye akili tupo wachache, wajinga wengi wanatuchafua”

 

Soma na hizi

Tupia Comments