Duniani

Ebola ilivyofanya staa wa Hollywood akatua ndani ya Nigeria kuitengeneza movie yake…

on

Kwa kipindi cha 2014 na 2015 Ebola imebeba Headlines kubwa sana… lakini ishu haikuwa Africa pekeyake, Dunia nzima ilibidi wakae macho kwa sababu ya watu wanavyovuka mipaka ya nchi, ikafanya kwa upande mwingine kuidhibiti Ebola iwe sio kitu kidogo !!

danny-glover

Staa kutoka Marekani, Danny Glover katua Nigeria kwa kazi moja tu !! kama wewe ni fan wa nguvu damdam na movie kali kutoka Hollywood Marekani, jina la staa huyo sio geni…. kwenye list ya movie kali ziko na hizi hapa mtu wangu >>> ‘Legendary’ (2010- ndani yumo na John Cena pia), pamoja na movie ya ‘Rage’ ambayo amefanya na staa mwingine Nicolaus Cage (ilitoka mwaka 2014).

Taarifa ikufikie kwamba mwigizaji huyo Danny Glover tayari katua Nigeria usiku wa September 08 2015 kwa ajili ya kuandaa hiyo Movie ambayo itakuwa inahusu masuala ya Ebola, jina lake itaitwa ’93 Days’ ambayo ndani yake kutakuwa na story inayowahusu watu waliojitolea kupambana na Ebola.

tim-reid-close-up

Tim Reid

Kwenye list ya Mastaa watakaoigiza Movie hiyo yupo pia Tim Reid kutoka Hollywood Marekani pamoja na mastaa wengine kutoka Nigeria na Africa.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments