Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuendelea kusaidia mamlaka za serikali za mitaa nchini na kwa gawio walilotoa kwa serikali na kuwasii wafanye bidii zaidi ili kuweza kuchangia zaidi pato la serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Dkt. Mpango alitoa wito huo wakati alipotembela banda la benki hiyo katika
Mkutano Mkuu wa 37 Jumuia ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaoendelea jijini Arusha. NBC Bank ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo ambao ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais.
Akizungumza na uongozi wa benki hiyo, Dkt. Mpangoa lipongeza benki hiyo kwa kuendelea kusaidia miradi inayolenga kuzisaida mamlaka za serikali za mitaa na kukuzamaendeleo katika ngazi ya msingi.
“Napongeza hatua nzuri ya NBC kufikia kiwango cha kutoa huduma jumuishi, lakini bado ninaendelea kusisitiza dhamira ya serikali kuendelea na mipango mkakati ya kutoa huduma za kifedha nafuu ili watanzania wengi waweze kufaidi. Wito huu nautoa kwa taasisi za kifedha zote nchini ili ziweze kusaidia Watanzania kadiri iwezekanavyo lengo likiwa ni kuwawezeshawaweze kuongeza mitaji wao na kuunda uchumi jumuishi.” Alisisitiza.
Kwa upande wake, Elibariki Masuke, Mkurugenzi wa Biasharaza reja reja wa benki ya NBC ambaye alimwakilishaMkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alionyesha kuridhishwana uwepo wa uhusiano mzuri kati ya benki hiyo na ALAT hukuakiahidi kuendelea kushirikiana na jumuiya hiyo katika jitihadazake za kukuza utawala bora na maendeleo nchini. Piaalionyesha matumaini kuhusu uwezekano wa ushirikiano zaidikati ya taasisi hizo mbili.
“Tunafurahi kupokea sifa kama hizi na wito kutoka kwaMakamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. Tunatambua pia kazinzuri za mamlaka za serikali za mitaa katika kuongozamaendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Kazi yao nzuri imeendeleakuwanufaisha Watanzania wengi. Kama benki inayotumikiavizuri taifa letu, Benki ya NBC tunaahidi kusaidia na kutoasuluhisho la kibenki linalotokana na mahitaji.” Aliongeza.
Masuke alisema benki hiyo pia ni miongoni mwa walipa kodiwakubwa waliochangia zaidi ya TZS 66.5 bilioni kwenye hazinaya taifa mwaka kwa 2022.
Katika kipindi hicho hicho, Benki ililipa gawio la serikali lenyethamani ya bilioni 6 TZS. “Tuna furaha kuwa mshirika muhimuna mshiriki katika ajenda ya maendeleo ya kitaifa, natunahakikisha kuendelea kusaidia. Milango yetu inaendeleakuwa wazi ili kutumikia si tu serikali na watumishi wa ummalakini Watanzania wote kwa ujumla.”
Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za kielektroniki kwaHalmashauri za Wilaya na Miji katika ukusanyaji wa mapato nasuluhisho za malipo ambayo yanapunguza gharama za kifedha.
Uwezo huu unaimarishwa zaidi na mfumo wake wa malipo yaSerikali, mtandao wake mkubwa wa NBC Wakala, mashine zaPOS, na usimamizi wenye usalama katika malipo na ukusanyajikwa rahisi zaidi.
Benki hiyo hivi karibuni ilizindua huduma yake kibenki yakidigitali inayofahamika kama “NBC Connect” ambayo pamojana mambo mengine inalenga kurahisisha malipo kwa njiamtandao. Benki hito pia inatoa huduma mbalimbali za mikopoili kukidhi mahitaji ya taasisi, makampuni, na watu binafsi.
“Zaidi tunaendelea kuhusika katika miradi muhimu ya serikaliili kuongoza maendeleo ya kiuchumi ukiwemo mradi wa ujenziwa reli ya SGR. Pia tumekuwa tukisaidia vikundi maalum kamawajasiriamali, mnyororo wa thamani ya kilimo, AMCOS, Wamachinga, bodaboda, na makundi mengine,” Masukealisema.