KUKITHIRI kwa vitendo vya ukatili kwa Watoto nchini, Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana na Waziri wa Jinsià, Maendeleo na Makundi Maalum pamoja na Waziri wa Elimu Adolf Mkenda kuweka mkakati wa kushirikiana katika kukomesha vitendo hivyo.
Akizungumza leo mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Magaya amesema ushirikiano kati ya Jumuiya na Wizara hizo itasaidia kudhibiti vitendo hivyo.
Amesema ukatili dhidi ya watoto na wanawake hujitokeza katika njia tofauti tofauti. Inaweza kuwa kimwili, kingono au kifikra. Inaweza kufanyika mbele za watu, faraghani au mtandaoni na kutekelezwa na mpenzi au mtu mwingine yoyote.
Bila kujali unafanyika vipi, wapi na umetekelezwa nani au ni kwa sababu gani? Ukatili una madhara makubwa ya muda mfupi au muda mrefu.
Amesema, jumuiya hiyo ya wazazi ina wajibu wa kusimamia Elimu,malezi, maadili na tamaduni kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, amesema wameandaa Kongamano Maalum la Kitaifa la Malezi litakalo fanyika mapema mwaka huu.
Magaya amesema bado mazungumzo yanaendelea na wadau wengine ili kuibua mjadala wa kitaifa wa mmomonyoko wa maadili unaendelea kwa kasi kubwa hapa nchini na ukatili wa kijinsia na watoto unaoendelea.
“Jumuiya ya wazazi ina wajibu wa kuisimamia na kuitekeza sera ya Malezi ya watoto na vijana ya Taifa ya mwaka 1987 ambayo Kongamano hili inaenda kuibua mjadala wa uboreshwaji wa sera hii ili kwenda na nyakati za sasa lakini pia kuibua mjadala wa malezi mema unaozingatia maadili bila kupoteza utambulisho wa mila na tamaduni zetu za Kitanzania.“Amesena
Kikao hicho kimeudhuriwa na Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally Said ambae ndio mwenyeji wa Kongamano hilo litakalozinduliwa rasmi Kitaifa ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.