Kutoka nchini Nigeria, vyombo vya ulinzi vimeimarisha ulinzi kwenye viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi hiyo kwa kupima abiria, baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutangaza kuingia kwa ugonjwa wa Ebola nchini kwao wiki hii.
Waziri wa Afya wa Nigeria Isaac Adewole ameliambia Shirika la Utangazaji la CNN kwamba wamegundua watu takriban 17 waliokuwa wakisafiri wanakisiwa kufariki kwa virusi hivyo vya homa ya Ebola.
Inaelezwa kuwa miili ya watu hao itafanyiwa uchunguzi wa halijoto katika mipaka ya nchi hiyo.
“Tunaimarisha ulinzi, na wanaotokea DRC watakaguliwa na kusimamiwa na mamlaka husika baada ya kuondoka kwenye viwanja hivyo vya ndege, bandari na mipakani.” – Isaac Adewole
Msaada alioupata Mlemavu aliyekimbiwa na Mume na kuachiwa Mtoto