Top Stories

Ni urembo?!!Kapata chongo kisa kuchora tattoo

on

Mwanamitindo Catt Gallinger wa Ottawa Canada amepata madhara makubwa ya jicho na kuelezwa na madaktari kwamba anaweza kuwa chongo baada ya kwenda kuchora tattoo kwenye jicho hilo.

Imeelezwa kuwa binti huyu alikua anataka kuchora tattoo hiyo kwenye sehemu ya rangi nyeupe ya jicho hilo la kulia na suala hili likashindikana na kusababisha madhara hayo ambapo sasa jicho limekuwa la rangi ya purple na hata machozi yanatoka ya rangi hiyo ya purple.

Catt ameeleza kuwa amekwisha enda hospitali lakini hakuna mafanikio yaliyopatikana na kwamba mara ya kwanza aliwekea dawa ya antibiatic na baada ya dakika chache tu jicho likavimba na kufunga kabisa na baada ya hapo daktari akamwambia jicho lake limeharibika kabisa na kwamba linahitaji kutolewa kabisa.

Eyeball tattoo leaves woman crying purple tears and in agony

Eyeball tattoo leaves woman crying purple tears and in agony

Ulipitwa na hii? Dakika 215 za Yusuph Manji kujitetea kesi ya dawa za kulevya leo

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments