Angel Di Maria ataendelea Benfica kwa msimu zaidi,kulinga na vyombo vya habari vya kimichezo.
Di Maria, 36, atacheza mchezo wake wa mwisho wa kimataifa akiwa na Argentina katika fainali ya Copa America Jumapili dhidi ya Colombia. Lakini fowadi huyo, ambaye mkataba wake na Benfica ulimalizika mwezi uliopita, atasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu yake.
Di Maria alikataa kurejea katika klabu ya utotoni ya Rosario Central kwa sababu za kiusalama. Alihusishwa na kuhamia Inter Miami huku Besiktas pia wakionyesha nia ya kutaka kumsajili msimu huu wa joto.
Alijiunga tena na Benfica msimu uliopita wa joto na kufunga mabao 17 katika mechi 48 katika mashindano yote.