Mwaka huu umekuwa mzuri sana kwa mtu wetu Diamond Platnumz kwani amekuwa wa kupokea na kutajwa kwenye tuzo nyingi sana kwa mwaka huu wa 2015 na siku chache zilizopita Diamond Platumz alitajwa kuwania tuzo nyingine tena za kimatatifa MTV EMA 2015 jijini Milan Italy.
Headlines za Diamond Platnumz haziishii hapo, good news kwako mtu wangu msanii wetu wa Bongo Flava anazidi kuonyesha ubora wake kwenye nafasi mbalimbali za tuzo Africa… Diamond amepokea ushindi wa tuzo nyingine tena! African NAFCA Awards 2015 imemtaja Diamond kuwa Msanii wa mwaka anaependwa na wimbo wa ‘Nana’ umetajwa kuwa Wimbo wa mwaka unaopendwa!
Kupita page yao ya Instagram @africannafca walipost picha hizi za tuzo za Diamond Platnumz…
Na kupitia page yake ya Instagram, Diamond Platnumz amepost picha ya tuzo zake na ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wake…
Hongera na Big Up sana Diamond Platnumz!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos