Habari za Mastaa

Majibu ya Babu Tale baada ya ushauri wa Shigongo kwa Diamond Platnumz

on

March 31, 2017 Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Publishers Eric Shigongo aliyetoa ushauri kwa kumtaka Diamond Platnumz kuwa makini katika muziki wake, kwenye ujumbe wake Babu Tale amemtaka Shigongo kuheshimu biashara yao na heshima yao kwake.

Babu Tale ameyaandika haya..>>>Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kwenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…baada ya kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako.

“Siku zote nimekuheshimu na Sijawai kukuvunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wengine na watu mbalimbali….

“Tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tumekaa kimya… na kujifanya unazunguka eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?…..

“Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….

“Tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaweka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….

“Mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…tafadhali heshimu heshima yetu kwako?……”Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…..?” – Babu Tale.

On Air: ‘Babu Tale aliniambia nisitembee na Madee, Niende Ya Moto Band’ Rayvanny

Soma na hizi

Tupia Comments