Habari za Mastaa

Ishu ya P Diddy kusakwa na Polisi, kesi yake ni ugomvi ndani ya club !!

on

Sean Combs

Rapa maarufu na mmiliki wa Lebo ya Bad Boy Entertainment, Sean Combs maarufu kama P Diddy anasakwa na polisi kwa madai ya kumpiga shabiki mmoja katika hafla ya mchezo wa Super Bowl iliyofanyika nchini Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa mtandao kadhaa ikiwemo TMZ, mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Steven Donaldson ambaye ana umri wa miaka 45 alipigwa na mtu ambaye inasemekana ni P Diddy katika hafla ya Super Bowl iliyofanyika jumamosi usiku.

Mkanda mmoja wa video unamuonyesha Diddy akibishana na mtu huyo wakiwa wanatazamana uso kwa uso katika tukio ambalo Diddy anadaiwa kumpiga usoni kitendo ambcho hata hivyo hakikuonekana kwenye mkanda huo.

Steven Donaldson anadai kuwa Diddy alimpiga usoni kabla ya kuwaagiza walinzi wa hafla hiyo kumtoa nje huku yeye (Diddy)  akibakia kwenye eneo la tukio.

Steven aliishia kufungua mashtaka dhidi ya Diddy ambapo Polisi walifika eneo la tukio lakini hawakuweza kumkuta Diddy, alikuwa ameondoka tayari.

Miezi kadhaa iliyopita Diddy alidaiwa kupigana na Drake .

Miezi kadhaa iliyopita Diddy alidaiwa kupigana na Drake.

Polisi wa eneo la Scotsdale wamesema kuwa wanamtafuta Diddy ili wamhoji kuhusiana na tukio hilo na waweze kupata upande wake kabla ya kuamua kama atakuwa na shitaka la kujibu au la.

Chanzo cha ugomvi huo kinadaiwa kuwa malalamiko ambayo Steven aliyatoa baada ya kulipa kiingilio cha dola mia moja ili amuone P Diddy lakini star huyo hakujichanganya na watu wengine ambapo aliishia kukaa kwenye eneo VIP.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Diddy kukumbwa na tukio kama hili baada ya kudaiwa kumpiga ngumi rapa wa lebo ya Cash Money, Drake kwenye klabu moja ya usiku huko Miami baada ya kutokea ubishi baina ya wasanii hao juu ya haki miliki ya wimbo.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments