Michezo

Alichopost Samuel Eto’o Instagram kuhusu yeye na Didier Drogba

on

628x471Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ambaye alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao mawili ya Chelsea yaliyowaondoa Galatasary katika michuano ya UEFA Champions League jumanne iliyopita amepost picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa pamoja na mshambuliaji Didier Drogba – ambaye amekuwa mpinzani wake kwa muda mrefu katika medani za soka barani Afrika.

Eto’o alipost picha akiwa na Drogba na kuandika ujumbe wa kuonyesha uimara wa mahusiano yao pamoja na kuwa na upinzani kwenye soka.

etoo copy

Eto’o aliandika kifaransa: “Deux enfants d’une meme mère,…Mama Africa!!!”

Ambapo tafsiri yake ni “Watoto wa mama mmoja….Mama Africa!”

Tupia Comments