Top Stories

UPDATES: Polisi wamaliza upekuzi Makao Makuu ya ACT Wazalendo

on

Polisi wamekamilisha upekuzi wao Katika Ofisi ya ACT Wazalendo na kati ya vitu walivyoweza kuvipata ni pamoja na taaarifa ya Kamati ya Uongozi kwa Waandishi wa Habari (Press Release) ya Tarehe 21 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari “Kamati Kuu ya ACT Wazalendo Kujadili Hali Mbaya ya Uchumi wa Nchi, Mdororo wa Usalama na Kuminywa kwa Demokrasia”.

Pia wamepata taarifa ya Kamati Kuu kwa Waandishi wa Habari (Press Release) ya Tarehe 28 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari “Ushahidi Kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi wa Nchi Tofauti na Majigambo ya Serikali ya Awamu ya Tano”.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi Ado Shaibu, pia wameondoka na vifaa vya kielektroniki ikiwemo laptop na flash ambavyo vilivyotumika kuandaa taarifa hizo.

Ulipitwa na hii? ZITTO: ‘Sisi sio Mawakala wa Polisi, hawana mamlaka kuhoji Kamati Kuu”

Soma na hizi

Tupia Comments