AyoTV

AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto

on

Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori Diamond Platnumz amekua na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo wa bongo Hamisa Mobetto.

Stori zilianzia kwenye birthday party ya mama Diamond baada ya Hamisa kuonekana kuwa karibu na familia hiyo hasa dada wa Diamond lakini pia kuna picha iliyosambaa inaonyesha wawili hao kila mmoja amepiga picha kwa wakati wake lakini kwenye mazingira ya chumba yanayofanana.

Sasa August 2 2016 Leo Tena ya Clouds FM Diamond Platnumz ametolea ufafanuzi hiyo ishu na kusema “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana kwasababu yupo katika industry hizi za kufanya fashion, nimekua nikimjua muda mrefu kidogo na sikuwahi kuwa na matatizo nae yoyote sababu tumekuwa ni watu tu ambao tunaheshimiana …..” 

‘Sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikua kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na nafikiri hiyo imechangia kuingiza hayo maneno, kufanya video Tanzania mara nyingi huwa inaleta manenomaneno’

kupata full story ya Diamond akiongelea pia kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja bonyeza play hapa chini kumsikiliza akihojiwa na Geah Habib na Dahuu

ULIKOSA VIDEO YA NEY WA MITEGO KUMALIZANA NA BASATA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI 

Soma na hizi

Tupia Comments