Michezo

Angel Di Maria kumbe ana mipango tofauti na Manchester United..

on

diiiKocha wa Manchester United baada ya mchezo wa timu hiyo na Arsenal alitoa kauli ya kumtaka kiungo wa timu hiyo Angel Di Maria kuendelea kubaki kuitumikia klabu yake hiyo mbali ya kuwepo maneno mengi kuwa kiwango chake kimeshuka.

Mwenyewe ameibuka, anamtaka wakala wake ambaye anaitwa Jorge Mendes kumtafutia timu nyingine kwa ajili ya kwenda kucheza na yuko tayari kuondoka kwenye klabu hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Klabu za Barcelona, PSG na Juventus zimeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ingawa hajafanya mazungumzo yoyote na klabu hizo mpaka sasa.

Kwa mujibu wake Di Maria amesema amechoka kuitumikia klabu hiyo na anatamani kuona akicheza sehemu nyingine.

FBL-ENG-PR-ESP-MAN UTD-REAL MADRID-DI MARIA

Angel Di Maria akiwa na Kocha Louis van Gaal wakati aliposainiwa Man U mwaka 2014.

Di Maria alisainiwa Man United mwaka 2014 akitokea Real Madrid na kukabidhiwa jezi namba 7 ambayo ni ya kishujaa kwenye klabu hiyo, imevaliwa na mastaa wa soka kama George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments