Michezo

Di Maria aeleza tatizo lililomfanya ahame Man United na kujiunga na PSG……

on

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa ana kipiga katika klabu ya Manchester United kabla ya kutimkia klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Angel Di Maria, ameeleza sababu za yeye kulazimisha kuhama katika klabu ya Manchester United.

Angel-Di-Maria-602035

Di Maria ameeleza kuwa moja kati ya vitu vilivyomfanya asikubali kuendelea kubakia katika klabu ya Manchester United, ni falsafa za kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal ambaye alikuwa akimpanga nafasi ambayo yeye hakuwa na uzoefu nayo, hivyo ni kitu ambacho kilikuwa kinapelekea yeye na kocha huyo kupishana kauli wakati mwingine.

Angel-Di-Maria-339744

“Falsafa alizokuwa nazo Van Gaal ni moja kati ya sababu zilizonifanya nihame Manchester United ni ngumu kuzielewa falsafa zake, nilikuwa nikipishana naye kauli mara kadhaa. Nilizungumza na Blanc na ninaamini nitacheza namba yangu ambayo nilikuwa nacheza katika klabu ya Real Madrid hivyo nikahamia PSG” >>> Di Maria

Angel-di-Maria-Injury

Kiungo huyo alijiunga na Manchester United msimu uliomalizika, hivyo baada ya kwenda likizo hakurudi tena katika maandalizi ya msimu mpya, hadi pale Van Gaal alipokiri kuwa hafahamu alipo mchezaji huyo na siku kadhaa baadae uhamisho wake kwenda PSG hukawa umekamilika.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments