Michezo

Steven Gerrard ni mbaguzi wa watu weusi? kauli yake hii yamshangaza EL Hadji Diouf…

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Sabah ya Malaysia EL Hadji Diouf ameingia kwenye headlines baada ya siku kadhaa nyuma kuandikwa katika kitabu kipya cha kiungo wa kimataifa wa Uingereza anayeichezea klabu ya LA Galaxy ya Marekani Steven Gerrard.

EL Hadji Diouf aliingia katika headlines ya kitabu hicho ambacho ni cha maisha ya Steven Gerrard na kikubwa kilichomfanya azungumziwe ni baada ya Gerrard kuzungumzia ndani ya kitabu hicho kuwa angalau EL Hadji Diouf ndio aliwahi kumpenda.

footballer-El-Hadji-Diouf-spits-spitting

El Hadji Diouf

Stori ni kuwa EL Hadji Diouf hajaichukulia poa kauli ya Gerrard na hajafurahishwa nayo hata kidogo kwani kauli kama hiyo kwa upande wa EL Hadji Diouf ameichukulia tofauti na kusema kiungo huyo wa LA Galaxy ni mbaguzi wa rangi kwani inamaanisha hakuwahi kuwapenda wachezaji wengine weusi waliyowahi kusajiliwa na Liverpool.

Steven-Gerrard-of-England-holds-a-Say-No-To-Racism-sign

Steven Gerrard akiwa ameshika karatasi yenye ujumbe wa kupinga ubaguzi wa rangi.

“Gerrard hakuwahi kuwapenda watu weusi, kila wakati nilipokuwa na pishana nae hakuwahi kuthubutu kuniangalia machoni”>>> El Hadji Diouf

Steven Gerrard na EL Hadji Diouf ni wachezaji ambao wamewahi kucheza pamoja katika klabu ya Liverpool ya Uingereza kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2005, ambapo EL Hadji Diouf alihama Liverpool na kujiunga na klabu ya Bolton Wanderers kwa mkopo.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments