Ni Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo leo January 6, 2024 imewatangazia wanafunzi wa stashahada watakaodahiliwa mwezi Machi (March Intake) kwamba dirisha la maombi ya mikopo ya stashahada litafunguliwa kuanzia tarehe 15/01/2025 hadi tarehe 15/02/2025.
Wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo katika maeneo matano ya kipaumbele na wanafunzi wengine wenye udahili (admission) kwenye programu hizi na sio wanufaika wanashauriwa kutumia fursa hii kuomba mikopo kwa kuzingatia programu zilizomo katika orodha inapatikana kwenye tovuti hii kwa jina la ORODHA YA PROGRAMU ZA STASHAHADA 2024/2025.