Mrembo anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World 2016, Diana Edward amepata nafasi ya kuongea na AyoTV na kutueleza changamoto anazokutana nazo akiwa kwenye kambi ya Miss World Marekani ambapo yupo mpaka siku ya fainali za Miss World Dec18.
>>>’Changamoto nilizokutana nazo tangu nifike huku kwanza ni hali ya hewa, kuna baridi kali sana, kitu cha pili ni chakula, vyakula vyao huku ni ngumu sana kuvizoea kwasababu nimeshazoea vyakula vya Tanzania lakini nimeviweza na ninaendelea kuvizoea hivyohivyo…
Kitu kingine ni lugha, kuna watu wengine labda unakaa naye na hajui kingereza au kuna vitu vingine wanakuwa wanakueleza lakini kwasababu umezoea kiswahili inakuwa inakushinda’. – Diana
Video:Post kubwa leo kwenye Instagram, Diamond Platnumz na Zari kupata mtoto wa Kiume>>>