Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, imemuachia huru aliyekuwa Diwani wa Kata ya Isengule, Oscar Sangu (CHADEMA), Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, katika kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili yeye na wanachama wenzake watano.
Hukumu hiyo ilitolewa jana, Agosti 4, 2022 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Dunstan Ndunguru, baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani watuhumiwa.
Washitakiwa wengine ambao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2019 ni Lespisi Elias, Emanuel Sebastian Mzerani, Busiga Clement, January Katuhu na Mickson Makatare.