Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia leo Jumatano, Februari 1, 2023 huku bei ya dizeli, mafuta ya taa zikishuka.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Ewura, imeonyesha kuwa katika Jiji la Dar es Salaam dizeli, mafuta ya taa zimeshuka kwa Sh190/Lita na Sh142/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 4 Januari 2023 wakati bei ya rejareja ya mafuta ya petroli ikibakia ile ile.
Mikoa ya Kaskazini Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara bei za rejareja za Februari 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la tarehe 4 Januari 2023.
Kwa upande wa Mikoa ya Kusini Mtwara, Lindi, and Ruvuma, bei za rejareja za Februari 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zimeshuka kwa Sh118/Lita na Sh160/Lita, mtawalia ikilinganishwa na toleo la tarehe 4 Januari
2023.