Mtayarishaji wa muziki wa Amapiano Themba Sekowe, maarufu kwa jina la DJ Maphorisa amekamatwa kwa madai ya kumshambulia mpenzi wake, Thuli Phongolo.
Kwa mujibu wa City Press, mwigizaji huyo alifungua kesi na kueleza maelezo ya tukio hilo katika taarifa iliyoonekana kwenye chapisho hilo.
Alisema kisa hicho kilitokea Jumapili saa sita usiku baada ya kumkabili Maphorisa kuhusu mabishano waliyokuwa nayo siku ya Jumamosi.
“Nilimkabili ili tuzungumze kuhusu mabishano yetu yaliyotokea usiku uliopita wakati wa tafrija yake… Alinishika na kunipeleka kwenye balcony, na kunishika shingoni kwa fujo,” Thuli alisema kama alivyonukuliwa na chapisho hilo.
Gazeti hilo pia lilinukuu chanzo ambacho kilifichua kuwa hii haikuwa mara ya kwanza kwa wanandoa hao kugombana.
“Walipigana mapema Desemba baada ya shutuma za kutokuwa mwaminifu. Walipigana tena mwezi uliopita lakini hawakufika kituo cha polisi.”
Awali Thuli alikana kuwa na uhusiano na Maphorisa. Wawili hao walizua tetesi za uchumba mnamo 2021 wakati video yao wakicheza dansi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Huku watu wakiendelea kukisia kuwa walikuwa wapenzi, Thuli alitumia ukurasa wake wa Twitter kuzima uvumi huo.
TAZAMA:HILI NDIO ENEO AMBALO NYAMA YA PANYA NI GHALI KULIKO KUKU