Habari za Mastaa

Dj wa Amapiano ‘Dbn Gogo’ kutua Tanzania, kuinogesha Elements DAR

on

Mbali na kwamba South Africa bado wanaendelea kupeta kwenye vichwa vya habari Duniani kwa utoaji wa ladhaa tofauti ya muziki wao unaotamba kwa jina la Amapiano.

Sasa time hii ni zamu ya wakazi wa Dar es Salaam kupata kile kinachostahili kutoka kwa Dbn Gogo ambae anatarajia kutoa burudani Ijumaa hii 24th.

Staa huyo atawaburudisha mashabiki ama wapenzi wa muziki wao kwa masaa yasiyopungua matatu jukwaa litakalofungwa Elements Masaki Dar es Salaam.

Miongoni mwa vitu vilivyompa umaarufu na kujulikana zaidi kufanikisha collabo hizo ambazo kwasasa zinapeta kwenye Radio mbalimbali  zikiwemo Dakiwe, Khuza Gogo, Bambelela, Possible na nyinginezo.

Possible — DBN Gogo X Musa Keys X Dinho X Lebza The Villain (Amapiano Now)

 

 

 

 

 

Tupia Comments