Leo January 2, 2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema inatarajia kusajili walipa kodi milioni moja kwa mwaka 2018 huku wakiwa na walipa kodi milioni 2.5 katika daftari la walipa kodi la sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Kodi za ndani wa Mamlaka hiyo, Elijah Mwandumbya amesema hatua hiyo inatokana na uzinduzi wa kampeni ya usajili wa walipa kodi. Ameongeza kuwa katika kampeni hii mwaka wa fedha 2017/2018 wamepanga kusajili walipa kodi milioni moja nchini kote.
Amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha wanatarajia kukusanya Sh. bilioni 44 ikiwa ni kodi ya majengo maeneo yote nchini na kwamba katika michezo ya kubahatisha mamlaka hiyo inatarajia kukusanya kodi sh. bilioni 25. Kuhusu usajili wa TIN, amesema ni bure hivyo wananchi hawapaswi kulipa kwa yeyote.
“Kwa walipa kodi wadogo wanaostahili kulipa kodi kwa makadirio badala ya kutayarisha mahesabu, robo ya kwanza ya malipo watailipa ndani ya siku 90 kuanzia waliposajiliwa.” -Mwandumbya
BREAKING: TRA kuanza kumchunguza Kakobe, “nina hela kuliko Serikali”
“Kakobe asifanye kanisa lake kichaka cha kufanyia siasa” – RC Gambo